Tiba

Idara ya Tiba inahusisha Bodi mbali mbali kama vile, Bodi ya Madaktari, Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi, Bodi ya Afya ya Jamii na Mazingira, Bodi ya Wakala wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bodi ya Wakala wa Chakula na Dawa, Bodi ya Afya ya Akili, Baraza la Wauguzi na Wakunga na Ofisi ya Muuguzi Mkuu Kiongozi. Pia, idara hii inahusika kwa Kupandisha hadhi Hospitali za Vijiji kuwa za Wilaya na Wilaya kuwa za Mkoa.

Miongoni mwa Huduma zinazotolewa na Idara ya Tiba ni:-

  • Udhibiti wa Kemikali, Chakula, Dawa na Vipodozi.
  • Huduma za uchunguzi wa Maabara na Mionzi.  
  • Huduma za matibabu ambayo inajumuisha (Huduma za Upatikanaji, utunzaji na usambazaji wa dawa)
  • Huduma za Mpango wa Damu salama.

Katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama, Wizara kupitia Kitengo cha Damu Salama imeendelea kukusanya, kuchunguza, kuhifadhi na kusambaza damu katika hospitali tofauti nchini. Wizara kwa kushirikiana na taasisi nyingine imeendesha mabonanza ya uchangiaji damu ili kuhakikisha inakuwepo damu ya kutosha katika hospitali zote nchini.

Loading